Tuesday 26 August 2014

JINSI YA KULIMA UYOGA NA KUONGEZA KIPATO CHA ZIADA



Uyoga ni chakula kizuri sana na chenye virutubisho vingi vinavyohijika katika mwili wa mwanadamu, Wataalumu wengi wa afya na tiba wanautumia katika kutibu magonjwa mbalimbali kwa mwanadamu, Tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa uyoga unavitamini za kutosha pamoja na protini.


 Miaka ya karibuni, utaalamu wa kuotesha uyoga umeanza hapa Tanzania baada ya watu kutilia maanani lishe bora ya protini na manufaa mengine ya zao hilo. Kwa kuwa uyoga upo wa aina mbalimbali, usitawishaji wake pia hutofautiana katika mahitaji yake, ikiwa ni pamoja na hali ya hewa, malighafi za kuoteshea, pia uyoga una soko kubwa na unaweza kumuongezea kipato mkulima kwa kuuza kwa kuwa unahitajika sana na watu wa lika zote pia unaweza kutumiwa kwa namna mbalimbali,kama vile chakula nk.



 Hata hivyo ni wananchi wachache tu wanaojua jinsi ya kuulima inavyopaswa na pia ni wachache wanaoweza kutofautisha aina mbalimbali za uyoga na upi unafaa kuliwa na upi haufai kwa kuliwa. Mama Witness M. Marwa wa Mazimbu Morogoro Tanzania ni kati ya wakulima wachache wanaujua jinsi ya kulima uyoga kitaalam, pia anajua kutofautisha uyoga unaofaa na usio faa kwa kulimwa. Pia ni kati ya wakulima wazoefu katika manispaa ya morogoro ambao wananufaika na kilimo cha uyoga.


Anaanza kuueleza kuwa ,  kwa Tanzania aina zinazofaa ni zile ambazo hustawi vizuri, kwenye maeneo ya joto la wastani wa nyuzi joto 20C hadi 33C. Aina hizi za uyoga pia uhitaji hali ya unyevu hewani (moisture) wa kiasi cha asilimia 75%. Kwa mfano uyoga aina ya mamama.

                            Mfano wa Ujenzi wa banda uyoga



















UOTESHAJI WA UYOGA


Ikiwa unahitahitaji kuanza kuotesha uyoga, inabidi kwanza uwe na chumba chenye paa ambalo litazuia jua, mvua, na vumbi. Chumba hiki ni vyema kiwe na sakafu inayohifadhi unyevunyevu pamoja na sehemu ya giza ambayo ni muhimu kwa kuotesha utando wa uyoga. Mkulima










Mara Nyingi mbegu za uyoga huzalishwa kwenye maabara zenye vifaa vinavyowezesha kuotesha mbegu hizo bila kuchafuliwa au kuchanganyika na vimelea kama bakteria, ukungu au jamii

nyingine za uyoga ambazo haziliwi.



UHIFADHI WA UYOGA

i) Unaweza ukauweka uyoga kwenye mifuko ya karatasi na kuhifadhi kwenye jokofu.
ii) Unaweza ukauanika juani hadi ukauke na kuweka kwenye mifuko ya nailoni liyofungwa vizuri ili isipitishe hewa na unyevu.

SOKO LA UYOGA
i) Watu wengi hupenda uyoga mbichi uliotoka shambani wakati huo huo kama kitoweo, kwa kutumia kama nyama, samaki, au kama kiungo.
ii) Unaweza kuuza uyoga mbichi kwa bei ya shilingi 8000/= hadi 15000/= kwa kilo kwa uyoga aina ya mamama.
Pia unaweza kuuza nje ya nchi ikiwa uyoga wako ni kiasi kikubwa na uko katika viwango vinavyo kubalika kimataifa.


MAMBO YA KUZINGATIA
Uzalishaji wa uyoga huzingatia sana hali ya hewa na vifaa ulivyonavyo, hivyo basi, kabla hujachagua aina ya uyoga unaotaka kupanda pata ushauri kwa wataalamu walio
karibu nawe.

Ukishanunua mbegu, kama hupandi kwa muda huo, hakikisha umehifadhi mbegu hiyo kwenye jokofu. Kama huna jokofu la kuhifadhia, nunua mbegu baada ya kuandaa kila kitu. Hata hivyo, uotaji wa mbegu huwa mzuri kama zitakaa nje ya jokofu kwa siku mbili.

Mbegu za uyoga huwekwa ndani ya chupa yenye ujazo wa mililita 300, waweza kutumia chupa moja katika kupanda kwenye kilo 15 ya mali ghafi ya kuoteshea. Hakikisha
unamaliza mbegu yote iliyo ndani ya chupa kwani ikibaki itapata maambukizo ya vimelea.
Hakikisha unaponunua mbegu iwe ni nyeupe. Mbegu ambayo siyo nyeupe ni dalili za maambukizo ya vimelea vingine na hivyo haifai kwa kupanda.

Hakikisha chumba cha kupandia ni kisafi na hakipati vumbi toka nje ili kuzuia maambukizo ya magonjwa ya uyoga.

Usimwagilie uyoga maji yasiyochemshwa kwani maji hayo mara nyingi si salama. Yaweza kusababisha vimelea vingine kuota, kwani uyoga ni dhaifu kuhimili ushindani wa
vimelea.

Pia waweza kusababisha magonjwa ya uyoga ambayo kutibu kwake kunahitaji kutumia dawa za viwandani ambazo ni sumu na hivyo kusababisha madhara kwa mlaji. Unaweza kupata faida nyingi kutokana na uzalishaji wa uyoga,

FAIDA ZA UYOGA:-
Lishe kama protini inayolingana na ile ipatikanayo kwenye maziwa, samaki na kunde. Pia utapata vitamini B, C, na D, na madini ya joto, phosphoras, chuma na potashi.

Uyoga husadikika kutibu maradhi kama kifua kikuu, kisukari, moyo, shinikizo la damu na figo.

Masalia ya mazao hutumika katika kuzalishia uyoga, na baada ya kilimo cha uyoga yanaweza kutumika kama mbolea asili kwa kilimo cha bustani. Masalia ya kilimo cha uyoga pia hutumika kama chakula cha mifugo kama ng’ombe.

Kilimo hiki huhitaji eneo dogo sana la ardhi na kiasi kidogo cha maji, hivyo hupunguza tatizo la ukosefu wa ardhi na ugomvi katika jamii ambao unatokana na tatizo hilo.

  Kilimo hiki ni njia nyepesi ya kutoa ajira kwa familia kutokana na gharama ndogo, teknolojia rahisi inayotumika na pato lake ni kubwa, hivyo kupunguza utegemezi kwa familia na umaskin pia hasa kwa atayetilia maanani na mkazo katika kulima uyoga. 

Makala hii imeandikwa na Magesa Melkory M, Kwakushirikiana na Mama Witness M. Marwa mkulima wa uyoga MOROGORO TANZANIA.

21 comments:

  1. Thanks for presenting this artical.. it is good and open new chance for agriculture bussiness, but try to make some review before posting to minimize writing errors..

    ReplyDelete
  2. Nashkuru sana kwa somo zuri,Naitaji izo mbegu za uyoga ntazipata wapi? namba yangu ni +255764212469, na E-mail ni nalusaka@gmail.com

    ReplyDelete
  3. Nimefurahi kusoma ujumbe huu mzuri. ...naomba kujua soko ili niweze kuzalisha uyoga na kuuza huko. ..email
    Pamagilapeter@gmail.com namba ya simu 0717437108

    ReplyDelete
  4. Nimefurahi kusoma ujumbe huu mzuri. ...naomba kujua soko ili niweze kuzalisha uyoga na kuuza huko. ..email
    Pamagilapeter@gmail.com namba ya simu 0717437108

    ReplyDelete
  5. Asante sana kwa elimu nzuri ya ujasiriamali.
    Ningalipenda kupata mawasiliano nawe maana ninahitaji elimu zaidi.
    Namba yangu 0655142118 .......email deodatusa@gmail.com

    ReplyDelete
  6. Asante sana kwa elimu nzuri ya ujasiriamali.
    Ningalipenda kupata mawasiliano nawe maana ninahitaji elimu zaidi.
    Namba yangu 0655142118 .......email deodatusa@gmail.com

    ReplyDelete
  7. Soko la uyoga liko vp sababu nataka kuanza kulima uyoga, please contact me gideonaidan63@gmail.com

    ReplyDelete
  8. Are you suffering financially or do you need an urgent cash to pay your bills? And you want to take the risk of transforming your own life. Try and get your ATM blank card today and be among the lucky one's who are benefiting from this card. This ATM card is set capable of hacking into any ATM machines anywhere in the world. I have to know about this blank ATM card when I was looking for work online about a month ago. It has really changed my life forever and now I can say I'm rich because I am a living testimony. The less money I get in a day with this card is $3,000. Even now and then keep pumping money into my account. Although the card is illegal but there is no risk of being caught. It is programmed in such a way that it cannot be tracked and also has a technique that makes it impossible for the CCTV camera to detect you when using it. For details on how to get yours today contact speedhackersnetwork001@gmail.com

    ReplyDelete
  9. Je, wewe ni matatizo ya kifedha au unahitaji fedha haraka ya kulipa bili yako? Na unataka kuchukua hatari ya kubadilisha maisha yako mwenyewe. Jaribu na kupata ATM tupu kadi yako leo na kuwa miongoni mwa bahati ya mtu ambaye ni kunufaika na kadi hii. Kadi hii ATM ni kuweka uwezo wa Hacking katika mashine yoyote ATM popote duniani. Nina kujua kuhusu kadi hii tupu ATM wakati mimi nilikuwa kutafuta kazi online kama mwezi mmoja uliopita. Ni kweli iliyopita maisha yangu milele na sasa siwezi kusema mimi nina tajiri kwa sababu mimi ni ushahidi hai. fedha kidogo mimi kupata katika siku na kadi hii ni $ 3,000. Hata sasa na kisha kuweka kusukumia fedha katika akaunti yangu. Ingawa kadi ni kinyume cha sheria lakini hakuna hatari ya kuwa hawakupata. Ni iliyowekwa katika namna ambayo haiwezi kupatikana na pia ina mbinu ambayo inafanya kuwa vigumu kwa CCTV kamera ya kuchunguza wewe wakati wa kutumia hiyo. Kwa maelezo juu ya jinsi ya kupata yako leo mawasiliano speedhackersnetwork001@gmail.com

    ReplyDelete
  10. I was searching for loan to sort out my bills & debts, then i saw comments about blank ATM card that can be hacked to withdraw money from any ATM machines. I doubted thus but decided to give it a try by contacting {martinshackers22@gmail.com} they responded with their guidelines on how the card works. i'was assured that the card can withdraw $5000 instant & was credited with $500,000.00 so i requested for one & paid the purchasing fee to obtain the card. 18 hrs later, i was shock to see the delivery agency in my resident with a parcel{card} i signed and went back inside and confirmed the card works after the agent left. This is no doubts because i have the card & has made used of the card.

    ReplyDelete
  11. Je eneo kama mwanza linafaa kwa kilimo hiki?

    ReplyDelete
    Replies
    1. VIP tunaweza organize tukaanzisha kilimo hichi maaana hata mm nipo mwanza

      Delete
  12. Je eneo kama mwanza linafaa kwa kilimo hiki?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tunaweza organize tukafanya kilimo hichi, maana hata mm nipo mwanza

      Delete
  13. Nashukuru sana kwa Makala Nzuri.
    Natamani kujua zaidi juu ya kilimo cha Uyoga.Tafadhali naomba mawasiliano yako.Mimi Naitwa David Peter na namba yangu ya simu ni 0767484549 pia barua pepe ni ferdavy@gmail.com

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hakika ni zao lenye faida kubwa kiafya, kukuza kipato na kutunza mazingira.
      Tangu nimeanza kilimo hiki ni zaidi ya miaka mitatu sasa sijajuta.Tunauza uyoga mkavu na mbichi, mbegu bora,Tunatoa mafunzo na ushauri,uanzishwaji na usimamizi wa miradi ya Uyoga.
      Tunapatikana Dar es Salaam.
      Twitter/Instagram/Facebook: Hertu Farms
      Simu: 0783182632/0713600915
      Whatsup: 0757315931
      E-mail: hertufarms@yahoo.com

      Delete
  14. Hakika ni zao lenye faida kubwa kiafya, kukuza kipato na kutunza mazingira.
    Tangu nimeanza kilimo hiki ni zaidi ya miaka mitatu sasa sijajuta.Tunauza uyoga mkavu na mbichi, mbegu bora,Tunatoa mafunzo na ushauri,uanzishwaji na usimamizi wa miradi ya Uyoga.
    Tunapatikana Dar es Salaam.
    Twitter/Instagram/Facebook: Hertu Farms
    Simu: 0783182632/0713600915
    Whatsup: 0757315931

    ReplyDelete
  15. Somo zuri sana. Nelipenda kwa kweli. Na mimi napenda nipate ujuzi zaidi ili niweze kilima zao la uyoga.
    Simu:0742323121

    ReplyDelete
  16. Somo zuri sana. Nimelipenda kwa kweli. Na mimi napenda nipate ujuzi zaidi ili niweze kulima zao la uyoga.
    Simu:0742323121

    ReplyDelete
  17. Je! unataka kununua figo, viungo vya mwili au unataka kuuza yako
    figo au viungo vya mwili? Je, unatafuta fursa ya kuuza
    figo yako kwa pesa kutokana na kuharibika kwa kifedha na hujui la kufanya, basi wasiliana nasi leo na tutakupa kiasi kizuri cha pesa $500,000 dola kwa Figo yako. Jina langu ni Daktari Patricia Marie na mimi ni Daktari Bingwa wa Mishipa ya Fahamu katika MAX HEALTH CARE Hospitali yetu ina utaalam wa Upasuaji wa Figo na pia tunashughulika na ununuzi na upandikizaji wa figo na wafadhili anayeishi na sambamba. Tunapatikana India, USA, Malaysia, Singapore. Japani.

    Tafadhali tujulishe ikiwa una nia ya kuuza au kununua figo au
    Organs tafadhali usisite kuwasiliana nasi kwa na kupitia barua pepe.

    Barua pepe: maxhealthcare406@gmail.com

    Kila la heri
    MKURUGENZI MKUU WA TIBA

    ReplyDelete