Thursday, 15 December 2016

PANYA WA SUA WANAVYOPATA MAFUNZO MPAKA WANAPATA WANATEGUA MABOMU

Panya wanapata shule kuweza kutambua vitu mbalimbali kama vile mabomu yaliofukiwa ardhini,vimelea ya magonjwa kama vile TB na vitu vingine kuwafanya wanakuwa jasiri, mpaka anahitimu nakupatia chet hadi anafikia ktk shahada ya kwanza yaani degree. angalia hiyo video chini hapo utaona



Tuesday, 26 August 2014

JINSI YA KULIMA UYOGA NA KUONGEZA KIPATO CHA ZIADA



Uyoga ni chakula kizuri sana na chenye virutubisho vingi vinavyohijika katika mwili wa mwanadamu, Wataalumu wengi wa afya na tiba wanautumia katika kutibu magonjwa mbalimbali kwa mwanadamu, Tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa uyoga unavitamini za kutosha pamoja na protini.


 Miaka ya karibuni, utaalamu wa kuotesha uyoga umeanza hapa Tanzania baada ya watu kutilia maanani lishe bora ya protini na manufaa mengine ya zao hilo. Kwa kuwa uyoga upo wa aina mbalimbali, usitawishaji wake pia hutofautiana katika mahitaji yake, ikiwa ni pamoja na hali ya hewa, malighafi za kuoteshea, pia uyoga una soko kubwa na unaweza kumuongezea kipato mkulima kwa kuuza kwa kuwa unahitajika sana na watu wa lika zote pia unaweza kutumiwa kwa namna mbalimbali,kama vile chakula nk.



 Hata hivyo ni wananchi wachache tu wanaojua jinsi ya kuulima inavyopaswa na pia ni wachache wanaoweza kutofautisha aina mbalimbali za uyoga na upi unafaa kuliwa na upi haufai kwa kuliwa. Mama Witness M. Marwa wa Mazimbu Morogoro Tanzania ni kati ya wakulima wachache wanaujua jinsi ya kulima uyoga kitaalam, pia anajua kutofautisha uyoga unaofaa na usio faa kwa kulimwa. Pia ni kati ya wakulima wazoefu katika manispaa ya morogoro ambao wananufaika na kilimo cha uyoga.


Anaanza kuueleza kuwa ,  kwa Tanzania aina zinazofaa ni zile ambazo hustawi vizuri, kwenye maeneo ya joto la wastani wa nyuzi joto 20C hadi 33C. Aina hizi za uyoga pia uhitaji hali ya unyevu hewani (moisture) wa kiasi cha asilimia 75%. Kwa mfano uyoga aina ya mamama.

                            Mfano wa Ujenzi wa banda uyoga



















UOTESHAJI WA UYOGA


Ikiwa unahitahitaji kuanza kuotesha uyoga, inabidi kwanza uwe na chumba chenye paa ambalo litazuia jua, mvua, na vumbi. Chumba hiki ni vyema kiwe na sakafu inayohifadhi unyevunyevu pamoja na sehemu ya giza ambayo ni muhimu kwa kuotesha utando wa uyoga. Mkulima










Mara Nyingi mbegu za uyoga huzalishwa kwenye maabara zenye vifaa vinavyowezesha kuotesha mbegu hizo bila kuchafuliwa au kuchanganyika na vimelea kama bakteria, ukungu au jamii

nyingine za uyoga ambazo haziliwi.



UHIFADHI WA UYOGA

i) Unaweza ukauweka uyoga kwenye mifuko ya karatasi na kuhifadhi kwenye jokofu.
ii) Unaweza ukauanika juani hadi ukauke na kuweka kwenye mifuko ya nailoni liyofungwa vizuri ili isipitishe hewa na unyevu.

SOKO LA UYOGA
i) Watu wengi hupenda uyoga mbichi uliotoka shambani wakati huo huo kama kitoweo, kwa kutumia kama nyama, samaki, au kama kiungo.
ii) Unaweza kuuza uyoga mbichi kwa bei ya shilingi 8000/= hadi 15000/= kwa kilo kwa uyoga aina ya mamama.
Pia unaweza kuuza nje ya nchi ikiwa uyoga wako ni kiasi kikubwa na uko katika viwango vinavyo kubalika kimataifa.


MAMBO YA KUZINGATIA
Uzalishaji wa uyoga huzingatia sana hali ya hewa na vifaa ulivyonavyo, hivyo basi, kabla hujachagua aina ya uyoga unaotaka kupanda pata ushauri kwa wataalamu walio
karibu nawe.

Ukishanunua mbegu, kama hupandi kwa muda huo, hakikisha umehifadhi mbegu hiyo kwenye jokofu. Kama huna jokofu la kuhifadhia, nunua mbegu baada ya kuandaa kila kitu. Hata hivyo, uotaji wa mbegu huwa mzuri kama zitakaa nje ya jokofu kwa siku mbili.

Mbegu za uyoga huwekwa ndani ya chupa yenye ujazo wa mililita 300, waweza kutumia chupa moja katika kupanda kwenye kilo 15 ya mali ghafi ya kuoteshea. Hakikisha
unamaliza mbegu yote iliyo ndani ya chupa kwani ikibaki itapata maambukizo ya vimelea.
Hakikisha unaponunua mbegu iwe ni nyeupe. Mbegu ambayo siyo nyeupe ni dalili za maambukizo ya vimelea vingine na hivyo haifai kwa kupanda.

Hakikisha chumba cha kupandia ni kisafi na hakipati vumbi toka nje ili kuzuia maambukizo ya magonjwa ya uyoga.

Usimwagilie uyoga maji yasiyochemshwa kwani maji hayo mara nyingi si salama. Yaweza kusababisha vimelea vingine kuota, kwani uyoga ni dhaifu kuhimili ushindani wa
vimelea.

Pia waweza kusababisha magonjwa ya uyoga ambayo kutibu kwake kunahitaji kutumia dawa za viwandani ambazo ni sumu na hivyo kusababisha madhara kwa mlaji. Unaweza kupata faida nyingi kutokana na uzalishaji wa uyoga,

FAIDA ZA UYOGA:-
Lishe kama protini inayolingana na ile ipatikanayo kwenye maziwa, samaki na kunde. Pia utapata vitamini B, C, na D, na madini ya joto, phosphoras, chuma na potashi.

Uyoga husadikika kutibu maradhi kama kifua kikuu, kisukari, moyo, shinikizo la damu na figo.

Masalia ya mazao hutumika katika kuzalishia uyoga, na baada ya kilimo cha uyoga yanaweza kutumika kama mbolea asili kwa kilimo cha bustani. Masalia ya kilimo cha uyoga pia hutumika kama chakula cha mifugo kama ng’ombe.

Kilimo hiki huhitaji eneo dogo sana la ardhi na kiasi kidogo cha maji, hivyo hupunguza tatizo la ukosefu wa ardhi na ugomvi katika jamii ambao unatokana na tatizo hilo.

  Kilimo hiki ni njia nyepesi ya kutoa ajira kwa familia kutokana na gharama ndogo, teknolojia rahisi inayotumika na pato lake ni kubwa, hivyo kupunguza utegemezi kwa familia na umaskin pia hasa kwa atayetilia maanani na mkazo katika kulima uyoga. 

Makala hii imeandikwa na Magesa Melkory M, Kwakushirikiana na Mama Witness M. Marwa mkulima wa uyoga MOROGORO TANZANIA.

Wednesday, 16 July 2014

UFUGAJI BORA WA KUKU WA KIENYEJI



 

Ulishaji
 Kuku wa kienyeji wanaweza kulishwa kwa kumia mahindi, mchele, na mabaki ya ugali. Vyakula hivi ni lazima vikaushwe vizuri na kusagwa vizuri. Ulishaji ni lazima ufanyike katika sehemu safi au kwa kutumia vyombo vilivyotengenezwa maalumu kwa ajili ya kulishia kuku.

Banda
Aidha kuku wawe wa kienyeji au wa kisasa, wanahitaji kuwa na banda zuri kwa ajili ya malazi na kuwalinda. Wanahitaji chumba chenye nafasi ya kutosha na kinachopitisha hewa ya kutosha. Ni lazima kuwawekea fito kwa kuwa ndege hupenda kupumzika juu ya fito. Ni lazima banda la kuku lifungwe vizuri nyakati za usiku ili kuzuia wanyama wanaoweza kuwadhuru kuku. Ni lazima liwe safi wakati wote ili kuzuia magonjwa kama vile mdondo na mengineyo. Usitumie pumba za mbao au nguo kuukuu kwenye viota vya kutagia kwani huchochea kuwepo utitiri na funza wa kuku. Inashauriwa kutumia mchanga laini.

Maji ya kunywa
Kuku wapatiwe maji safi. Ni lazima kuangalia mara kwa mara na kuyabadilisha maji. Kamwe usiwape kuku maji machafu.

Chanjo
Chanjo kwa mifugo ni lazima ili kuzuia mashambulizi ya magonjwa. Magonjwa yaliyozoeleka ni kama vile Mdondo, Kideri, Ndui ya kuku, na homa ya matumbo (typhoid). Chanjo kwa kawaida hutolewa mara moja kwa kila baada ya miezi miwili.

Uwekaji wa kumbukumbu
 Kumbukumbu zijumuishe aina ya ulishaji, namba ya uzalishaji, muda wa mwisho wa matumizi, kiasi cha malisho kwa kila siku, idadi ya vifo, na idadi ya mayai yaliyozalishwa.

Mwanzoni unahitaji nini?

Wafugaji walio wengi wanauliza wanahitaji nini katika hatua za awali ili kuweza kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku. Hii itategemea aina ya kuku uliochagua kufuga.

Ni busara kuwa na vifaa muhimu vinavyohitajika na viwe katika hali ya usafi kabla ya kuweka kuku bandani mwako. Kama unaanza na vifaranga, vifuatavyo ni vifaa muhimu vinavyohitajika kwa ajili ya vifaranga 200.

• Tengeneze banda zuri lenye joto na hewa ya kutosha wakati wote.
• Vyombo vinne (4) vya kunyweshea maji, hii ni katika wiki 2 za mwanzo na uongeze vyombo taratibu kulingana na kuku wanavyokua.
• Vyombo vinne (4) vya kulishia chakula, na viongezeke kulingana na kuku wanavyokua.
• Matandazo makavu na safi, inaweza kuwa maranda au mabua ya ngano.
• Pakiti moja au mbili za dawa ya Coccid (hii inapatikana katika maduka yote ya kilimo). Hata hivyo, utaratibu wa chanjo ni lazima ukamilishwe.
• Chakula cha vifaranga kiwe kimezalishwa na watengenezaji wanaoaminika au ikiwezekana tengeneza mwenyewe kwa kufuata maelekezo ya wataalam.

imeandaliwa na Melkiory Magesa M (Afisa Ugani/Kilimo na mifugo)


Thursday, 26 June 2014

SUA YAWA YA KWANZA KUGUNDUA CHANJO YA UGONJWA WA NDUI DUNIANI





ugonjwa wa ndui kwa kuku, baada ya siku 11 unavyoonekana kwa kuku

Tanzania imeingia katika vitabu vya kihistoria ya tiba baada ya Profesa Philemon Wambura kugundua chanjo ya ugonjwa wa ndui kwa kuku ambayo imetambuliwa kimataifa.Chanjo hiyo iitwayo ‘Fowl Pox TPV-1 strain,’ iliyofanyiwa utafiti kwa miaka 10 na ya kwanza kugunduliwa duniani, itaanza kutumika Afrika na dunia nzima hivi karibuni.

Wakati wa utiaji saini wa makubaliano na kampuni ya kimataifa  inayotengeneza dawa na chanjo mbalimbali za mifugo, MCI Sante Animale ya Morocco, Profesa Wambura alisema chanjo hiyo ni ya kwanza kukubalika kutumika kuzuia ugonjwa wa ndui ya kuku na ni rahisi kutumia ukilinganisha na chanjo nyingine zilizowahi kufanyiwa majaribio.“Ni fahari kwa Tanzania kuwa mgunduzi wa kwanza wa chanjo hii duniani, ni chanjo yenye ubora wa hali ya juu  na matumizi yake yataongeza uzalishaji wa kuku na kuongeza kipato,” alisema Profesa Wambura ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Tiba ya Wanyama wa Chuo cha Kilimo Sokoine (SUA).

Profesa Wambura alisema tofauti na chanjo nyingine, hiyo inaweza ikawekwa kwenye chakula au maji ya kunywa bila kupata usumbufu wa kuwakamata mmoja mmoja na kuweka dawa machoni kama ilivyozoeleka.Alisema chanjo hiyo ina sifa kubwa ya kuvumilia joto, jambo linaloifanya kuwa ni rafiki wa mazingira ya vijijini ambako hakuna umeme na ina uwezo wa kutambua iwapo kuku ana virusi vya ugonjwa wa ndui kwa kutumia damu ya kuku mwenyewe.

“Madhumuni yetu ni kuhakikisha chanjo hii inapatikana kwa bei nafuu ili hata wananchi wa kawaida wanufaike. Ndiyo maana itazalishwa kwa wingi ili iuzwe kwa bei nafuu,” alisema.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk Hassan Mshinda alisema ni fahari kubwa kuwa kazi ya mtafiti wa Kitanzania imeonekana na mataifa ya nje, jambo ambalo linatoa ari kwa watafiti wengine kufanya kazi zaidi.Alisema mradi  huo wa chanjo ya ndui ya kuku uliogharimu Sh205 milioni ni wa kimataifa na chanjo hiyo itasambazwa duniani kote kwa ushirikiano wa Costech na Kampuni ya MCI.

“Ni vizuri sasa tafiti za Kitanzania zinatumika badala ya kuhifadhiwa kwenye makabrasha bila faida yoyote. Ni kazi ya kujivunia hasa,” Mkuu wa Kitengo cha Uendelezaji wa Biashara wa MCI, Dk Baptiste Dungu alisema kampuni yake imefanya kazi na Profesa Wambura na kugundua kuwa utafiti wa chanjo yake una manufaa makubwa kwa sababu ni wa kwanza duniani.

Kwa kawaida ugonjwa wa NDUI YA KUKU, kuku huonekana na vipele vya rangi ya kijivujivu, kwenye ngozi yake, hasa kwenye upanga wa kichwa.


habari hii inapatikana pia, http://magesam.blogspot.com/


Thursday, 11 April 2013

JE KILIMO CHETU TANZANIA KINAKUWA?


Ni swali ambalo kila mtanzania atakiwa kujiuliza?
Kuwa kwa juhudu mabalimbali zifanyazo na serikali yetu,wadau mbalimbali wa kilimo na taasisi mbalimbali za kilimo,je kilimo chetu kinakuwa?